BIRMINGHAM:wanane wakamatwa kwa ugaidi Uingereza
31 Januari 2007Matangazo
Polisi nchini Uingereza, imewakata watu wanane kwa kushukiwa kujihusisha na ugaidi.
Watu hao walikamatwa katika mjini wa Birmingham, babada ya polisi kuendesha msakao katika mji huo dhidi ya watu wanajiuhusisha na vikundi vya kigaidi.
Hata hivyo mpaka sasa hakuna taarifa zaidi juu ya kukamatwa kwao.
Wiki iliyopita polisi waliendesha msako kama huo katika miji ya Yorkshire na maeneo ya kaskazini mwa Uingereza.