BETHLEHEM:Waziri wa Ujerumani ziarani Mashariki ya Kati | Habari za Ulimwengu | DW | 05.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BETHLEHEM:Waziri wa Ujerumani ziarani Mashariki ya Kati

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Frank Walter Steinmeier anaetembelea maeneo ya wapalestina amekutana na waziri wa fedha wa mamlaka ya Palestina bwana Fayyad.

Hayo ni mawasiliano ya kwanza ya ana kwa ana baina ya mjumbe wa ngazi ya juu ya serikali ya Ujerumani na mwakilishi wa serikali ya mseto ya wapalestina ya chama cha Hamas na chama cha Fatah.

Waziri Steinmeier pia anatarajiwa kufanya mafungumzo na rais wa mamlaka ya Palestina bwana Mahmoud Abbas baadae leo.

Bwana Steinmeier ataendelea na ziara yake ya mashariki ya kati, kwa kuitembelea Israel kesho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com