1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Uzio warefushwa Heiligendamm

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuw

Polisi nchini Ujerumani wameongeza urefu wa uzio wa usalama uliowekwa katika eneo la Heiligendamm kunakofanyika mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa nane yaliyostawi kiviwanda ulimwenguni G8.

Vyombo vyote vya majini vinapigwa marufuku kufika katika eneo la umbali wa kilomita 11 kutoka ufuo wa bahari kunakofanyika kikao hicho.

Maafisa wa usalama wameshapiga marufuku watu kuingia mjini na kuuzungushia uzio ulio na urefu wa kilomita 11.Wakazi wa mji huo pamoja na wafanyikazi wa mkahawa kunakofanyika kikao ndio wanaoruhusiwa kuingia katika eneo hilo.Takriban watu alfu 1 watapewa vitambulisho maalum ili kuruhusiwa kuingia.

Viongozi kutoka mataifa yaliyostawi kiviwanda ulimwenguni ya Uingereza,Ufaransa,Ujerumani,Italia,Japan,Urusi na Marekani wanahudhuria kikao hicho cha kilele mjini Heiligendamm kuanzia tarehe 6-8 mwezi huu.