BERLIN:Ujerumani yathibitisha kutekwa nyara mwananchi wake mwengine Afghanistan
19 Agosti 2007Matangazo
Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imethibitisha kuwa mjerumani mwengine ametekwa nyara nchini Afghanistan.
Mjerumani huyo mwanamke aliekuwa anafanya kazi kwenye shirika la kutoa misaada alitekwa ndani ya mkahawa na watu wanne waliokuwa na silaha.
Msemaji wa shirika hilo la misaada bwana Ulf Baumann pia amehibitisha juu ya kutekwa nyara mama huyo bila ya kutoa maelezo zaidiAmesema anachojua ni kwamba mama huyo alitekwa nyara ndani ya mkahawa.