BERLIN:Ujerumani yatafakari ombi la kupeleka ndege ya upepelezi Afghanstan | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Ujerumani yatafakari ombi la kupeleka ndege ya upepelezi Afghanstan

Serikali ya Ujerumani inatafakari ombi la NATO la kuipatia ndege ya upepelelezi Afghanstan.

Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya ulinzi wa Ujerumani uamuzi juu ya suala hilo utatolewa mapema mwakani na kwamba ndege hiyo inaweza kutumiwa katika nchi nzima ya Afghanstan.

Ujerumani imekuwa katika shinikizo za kuitaka iongeze muda wa kubakia wanajeshi wake katika sehemu zilizoko nje ya maeneo tulivu ya kaskazini nchini Afghanstan pamoja na kukisaidia kikosi cha ISAF kwenye eneo tete la kusini .

Kwa sasa kuna wanajeshi kiasi cha 3000 wa ujerumani nchini Afghanstan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com