1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Stoiber ajiondoa kwenye ulingo wa siasa

30 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLM

Mpinzani wa muda mrefu wa kansela Angela Merkel Edmund Stoiber amejiondoa katika uwanja wa siasa.Hatua hiyo imezidisha nguvu kwa kansela ingawa anakabiliwa na kibarua kigumu katika muungano.

Edmund Stoiber amejiuzulu waziri mkuu wa jimbo la Bavaria na kiongozi wa chama cha Kisosholisti CSU ambacho ni chama ndugu na kile cha Kansela Angela Merkel cha CDU.Chama cha CSU kimemchagua waziri wa uchumi na usafiri Erwin Huber kuwa kiongozi wa chama hicho huku Guenther Beckstein waziri wa mambo ya ndani wa Bavaria akichaguliwa kuwa waziri mkuu wa jimbo hilo.Stoiber mwenye umri wa miaka 66 alishindwa katika kinyanga’nyiro cha kuwania ukansela wa serikali kuu mwaka 2002.