BERLIN:Merkel ziarani Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 30.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Merkel ziarani Marekani

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekwenda Marekani kukutana na rais Gorge Bush kujadili masuala mbali mbali ikiwemo Uchumi.

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kusaini makubaliano yaliyoundwa kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani.

Watajadili pia kuhusu juhudi za kupambana na ongezeko la ujoto duniani na masuala mengine ya kimataifa kama vile hatma ya Kosovo na Afghanstan.

Haijakuwa wazi ikiwa viongozi hao watazungumumzia kuhusu mpango wa Marekani uliozusha utata wa kuweka ulinzi dhidi ya makombora katika nchi za Poland na jamhuri ya Czech.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com