1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Madereva wa treni wataka asilimia 30 nyongeza ya mshahara

Madereva wa treni wa nchini Ujerumani leo wamegoma kwa mara ya pili katika kipindi cha wiki moja kushinikiza madai yao ya nyongeza ya mshahara.

Chama kinachotetea maslahi ya wafanyakazi madereva wa treni nchini Ujerumani GDL kimesema kimeitisha mgomo huo kama isharara ya kutoku kubaliana na pendekezo la shirika la reli la Deutsche Bahn la hivi karibuni.

Shirika la Deutsche Bahn limetoa pendekezo la tano la malipo kwa madereva hao ikiwa ni pamoja na malipo ya mara moja ya Euro 2,000 na asilimia kumi ya ongezeko la mshahara.

Chama cha GDL kinataka madereva wa treni waongezewe asilimia 30 ya mshahara.

Mgomo huo uliodumu kwa saa tisa umeathiri zaidi usafiri wa mikoani.

Hali kama hiyo inaikumba sekta ya usafiri wa treni nchini Ufaransa ambako madereva wa treni wameanzisha mgomo wa saa 24.

Watetezi wa wafanyakazi wa treni nchini Ufaransa wameitisha mgomo huo kumshawishi rais Nicolas Sarkozy abadili mpango wake wa mageuzi katika malipo ya uzeeni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com