Berlin.Hatma ya Wajerumani wawili waliotekwa nyara haijulikani.
22 Machi 2007Matangazo
Serikali ya Ujerumani imerudia kueleza wasi wasi wake juu ya hatma ya Wajerumani wawili waliokamatwa nchini Iraq wiki sita zilizopita. Muda wa mwisho uliowekwa na wateka nyara hao umemalizika siku ya Jumanne, na hakuna taarifa juu ya hali ya mateka mwanamke mwenye umri wa miaka 61 na mwanawe mkubwa wa kiume.
Wateka nyara hao wanadai kuwa Ujerumani iondoe kabisa majeshi yake kutoka Afghanistan.
Kansela Angela Merkel amekataa madai hayo, akisema kuwa Ujerumani haitaruhusu kurubuniwa.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema kuwa serikali inafanya kila inaloweza ili kupata kuachiliwa huru kwa watu hao.