1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Bundestag lajadili juu ya kuongeza muda wa vikosi Afghanstan

1 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNg

Bunge nchini Ujerumani Bundestag linajadili juu ya kuongeza muda wa kubakia kikosi cha Ujerumani huko Afghanstan pamoja na kutuma ndege za kivita.

Wizara ya ulinzi imesema jeshi la Ujerumani halitahusika moja kwa moja kwenye mapambano lakini viongozi wa upinzani wanapinga suala hilo.

Bunge linatarajiwa kufikia uamuzi juu ya iwapo watatuma ndege hizo katika wiki zijazo.Mswaada huo hata hivyo unatarajiwa kupita kwani serikali ya mseto ina idadi kubwa ya viti bungeni.