BERLIN:Angela Merkel alaani uamuzi wa mahakama ya Libya
20 Desemba 2006Matangazo
Kansela Angela Merkel amelaani vikali uamuzi wa mahakama ya Libya wa kutoa huku ya kifo dhidi ya wauguzi watano wa Kibulgaria na daktari wa Kipalestina wanaotuhumiwa kuwaambukiza kimakusudi watoto zaidi ya 400 wakilibya virusi vya HIV.
Akizungumza akiwa ziarani huko Helsnki Merkel ameitaja hukumu hiyo kuwa ya kutisha na kuitolewa mwito serikali ya Libya kuingilia kati kesi hiyo.
Hii ni mara ya pili kwa watu hao kuhukumiwa kifo ambapo mara ya kwanza walipewa hukumu hiyo mwaka 2004 lakini mahakama kuu ya Libya ikapinga uamuzi huo na kuamuru kesi hiyo isikilizwe tena.
Kamishna wa sheria katika umoja wa Ulaya Franco Frattini pia amezungumzia kushutushwa kwake na uamuzi huo na kuitaka mahakama hiyo ifikirie tena hukumu hiyo.