1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Vyama tawala vyailaumu Marekani kuuza silaha mashariki ya kati.

31 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdY

Chama cha kansela wa Ujerumani Angela Merkel cha Christian Democrats pamoja na chama kishiriki katika serikali ya mseto cha Social Democrats vimeeleza wasi wasi wao kuhusu mipango ya Marekani ya kuuza silaha katika mataifa ya mashariki ya kati.

Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya kigeni ya bunge la Ujerumani , Ruprecht Polenz , ameliambia gazeti la kila siku la Frankfurter Rundschau kuwa mashariki ya kati tayari ni eneo la hatari na kwamba kuingia kwa silaha kali kutaliweka katika hatari zaidi.

Katibu mkuu wa chama cha Social Democratic Hebertus Heil amesema kuwa ni hatari kwa Marekani kutoa silaha kwa eneo ambalo halina usalama.