1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Uturuki yawekewa ngumu kujiunga na Ulaya

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2m

Kiongozi wa chama cha kihafidhina nchini Ujerumani cha Christian Social Union kwa mara nyengine tena amesema kwamba mazungumzo ya Umoja wa Ulaya na Uturuki juu ya kujiunga kwa nchi hiyo katika umoja huo yanapaswa kusimamishwa.

Edmund Stoiber amewaambia wajumbe wa chama chake kwenye mkutano huko Augsburg kwamba Uturuki inapaswa isiruhusiwe kujiunga na umoja huo hadi hapo itakapokubali kuitambuwa rasmi Cyprus.

Katika masuala ya ndani ya nchi Stoiber amemshutumu kiongozi wa cham cha Social Demokrat Kurt Beck kwa kutoonyesha mshikamano wa kutosha na Kansela Angela Merkel.

Stoiber amesema wabunge wa chama cha Social Demokrat ambacho kinaunda muungano mkuu wa serikali ya mseto na chama cha Christian Demokrat cha Merkel wamekuwa wakikwamisha miradi muhimu ya mageuzi.