1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Ulaya yakaribisha kuachiliwa kwa Ndayizeye

20 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZZ

Rais wa Umoja wa Ulaya ambayo ni Ujerumani hapo jana imekaribisha kuachiliwa kwa rais wa zamani wa Burundi Domitien Ndayizeye na watu wengine wanne wiki hii kufuatia madai ya kula njama za kupinduwa serikali ya nchi hiyo.

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imesema katika taarifa kwa niaba ya nchi wanachama 27 wa Umoja wa Ulaya kwamba kuachiliwa huko kunachangia kuleta mazingira mazuri ambayo yanaimarisha utawala wa sheria na asasi za kidemokrasia.

Imeongeza kusema kwamba Umoja wa Ulaya unatumai hatua hizo zinawakilisha hatua za kusonga mbele kuelekea demokrasia ambapo kwayo uhuru wa kujieleza unaheshimiwa.

Wakosoaji wa serikali ya Burundi wamesema kutuhumiwa kwa Ndiyezeye na wenzake kula njama ya kumuuwa Rais Pierre Nkurunziza na kuipinduwa serikali yake kumebuniwa na serikali ili kuzima upinzani.