1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani yaukaribisha uamuzi wa baraza la usalama kuhusu Darfur.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBd1

Ujerumani imeukaribisha uamuzi wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuweka wanajeshi 26,000 wa jeshi la kulinda amani la umoja wa Afrika na umoja wa mataifa katika jimbo lililokumbwa na vita la Darfur nchini Sudan.

Waziri wa mambo ya kigeni Frank-Walter Steinmeier amewaambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Nigeria Abuja , kuwa ukweli kuwa mataifa ya Afrika yanataka kuchukua majukumu mengi zaidi ni hatua muhimu.

Hata hivyo , serikali ya mseto inayoongozwa na kansela Angela Merkel imeondoa uwezekano wa kutuma wanajeshi zaidi wa Bundeswehr katika eneo hilo.

Msemaji mjini Berlin amewaambia waandishi wa habari kuwa Ujerumani itabaki na majumu yake ya hivi sasa ya kuwa na wanajeshi 200 ambao wanatoa huduma ya usafiri kwa majeshi ya umoja wa Afrika AU. Serikali ya Sudan imeahidi kutoa ushirikiano kamili kwa majeshi ya kulinda amani ya umoja wa mataifa na umoja wa Afrika. Wanajeshi wa kwanza wanatarajiwa kuwasili mwezi wa Oktoba.