BERLIN : Ujerumani ina wasi wasi na mzozo wa bei ya gesi | Habari za Ulimwengu | DW | 29.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Ujerumani ina wasi wasi na mzozo wa bei ya gesi

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani ameelezea wasi wasi wake juu ya mzozo wa bei ya gesi kati ya Belarus na kampuni ya taifa ya Urusi ya Gazprom.

Waziri huyo Michael Glos amezihimiza pande zote mbili kufikia muafaka haraka iwezekanavyo.Gazprom imetishia kukata usambazaji wa gesi kwa Belarus ifikapo tarehe Mosi Januari iwapo Belarus itakataa kukubali pendekezo la kupandishwa mno kwa bei ya gesi hiyo.

Serikali ya Ujerumani imewahakikishia watumiaji wa gesi kwamba hakuna tishio la usambazaji wa gesi nchini Ujerumani kwa sababu ni gesi kidogo tu ya Ujerumani hupitia Belarus.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com