1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Uchunguzi mpya kwa mauaji ya 1977

24 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC7h

Kunapangwa kuanzishwa uchunguzi juu ya madai kwamba asasi za usalama na ujasusi za Ujerumani zilizuwiya habari juu ya kuuwawa kwa mwendesha mashtaka wa serikali na magaidi wa sera za mrengo wa shoto miaka 30 iliopita.

Msemaji wa waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schäuble ametowa tangazo hilo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Berlin.

Madai yaliochapishwa na gazeti la Spiegel yanahusiana na mauaji ya mwaka 1977 ya mwendessha mashtaka mkuu wa serikali Siegfried Buback.Wanachama watatu wa kundi la Red Army walipatikana na hatia ya mauaji hayo.Ilikuwa ikiaminika lakini haikuwahi kuthibitishwa kwamba Buback aliuliwa na gaidi Christian Klar.

Lakini hivi sasa wapiganaji wawili wa zamani wa Red Army wamesema kwamba ni mtu mwengine Stefan Wichnievski ndie aliefyatuwa risasi zilizomuuwa Buback.