BERLIN : Picha za wanajeshi na bufuru kuchunguzwa | Habari za Ulimwengu | DW | 25.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Picha za wanajeshi na bufuru kuchunguzwa

Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani imesema inachunguza picha zinazoonyesha wanajeshi wa Ujerumani wakiwa na bufuru nchini Afghanistan.

Gazetu la Bild la Ujerumani limesema picha hizo zenye kuchafuwa mojawapo ikiwa imechapishwa katika ukurasa wake mbele imewaoynesha wanajeshi hao wa kulinda amani wa Ujerumani wakiwa katika mji mkuu wa Kabul mapema hapo mwaka 2003.Wanajeshi hao waliovalia sare walikuwa wamepiga picha na bufuru wakiwa katika gari lao la kijeshi.

Gazeti hilo limesema ilikuwa haijulikani bufuru hilo limetokea wapi au iwapo lilikuwa ni la Muafghanistan au kwamba lilikuwa la zamani wakati wa Urusi ilipokuwa ikiikalia kwa mabavu nchi hiyo katika miaka ya 1980.

Gazeti hilo pia halikusema vipi ilipata picha hizo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com