BERLIN : Olmert atowa heshima zake kwa wahanga wa Kiyahudi | Habari za Ulimwengu | DW | 12.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Olmert atowa heshima zake kwa wahanga wa Kiyahudi

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert akianza ziara ya siku mbili nchini Ujerumani leo ameweka shada la mauwa katika kituo cha treni cha Grünewald mjini Berlin ambapo ndipo walipoondokea maelfu ya Mayahudi wakati wakipelekwa kwenye makambi ya mateso wakati Maagamizi ya Mayahudi katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.Katika hotuba fupi amesema kile wangelichotaka Wayahudi milioni sita waliouwawa chini ya utawala wa Hitler kuliko kitu kingeni chochote kile ni kuwa na taifa la Israel lililo tafauti kabisa na uovu wa Manazi.

Olmert leo anatazamiwa kuwa na mazungumzo na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambapo agenda inatazamiwa kuwa suala la mpango wa nuklea wa Iran na matarajio ya kufufua mpango wa amani kati ya Israel na Wapalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com