BERLIN : Njama ya kuripua ndege ya abiria yazimwa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Njama ya kuripua ndege ya abiria yazimwa

Serikali nchini Ujerumani imefichua kile inachotuhumu kuwa njama iliozimwa ya kuripua ndege ya abiria.

Duru za usalama nchini Ujerumani zimesema kwa sharti ya kutotajwa jina kwamba ndege hiyo iliopangwa kuripuliwa ilikuwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Frankfurt ambapo ni mojawapo ya viwanja vya ndege vyenye harakati kubwa kabisa duniani.

Mojawapo ya duru hizo za usalama imethibitisha taarifa za vyombo vya habari nchini Ujerumani kwamba ndege iliokusudiwa ilikuwa ni ya shirika la ndege la Israel ya El Al.

Waendesha mashtaka wa serikali ya Ujerumani katika mji wa Karlsruhe wamesema wanawachunguza watuhumiwa sita. Gazeti la Ujerumani la Tagesspiegel limeripoti kwamba takriban wote wanaofanyiwa uchunguzi huo ni raia wa Jordan wenye asili ya Kipalestina.

Nyumba tisa zilipekuliwa katika mikoa ya Ujerumani ya magharibi ya Rhilenland-Palatinate na Hesse kuhusiana na uchunguzi huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com