1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Merkel akutana ma Abbas

23 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPD

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel ametoa mwito mwanajeshi wa Israel aliyetekwa nyara na wanamgambo wa kipalestina mwezi Juni mwaka jana aachiliwe huru.

Bi Merkel alikuwa akizungumza baada ya kukutana na rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, mjini Berlin hii leo.

Amesema kuachiliwa kwa mwanajeshi huyo kutasaidia matayarisho ya kuachiliwa huru wafungwa wa kipalestina na kusaidia pia kuboresha mahusiano baina ya Waisraeli na Wapalestina.

Kansela Angela Merkel anaunga mkono kuundwa kwa mataifa mawili ya Israel na Palestina yatakayoishi kwa amani.

´Lengo ni kufikia makubaliano ya kuundwa kwa mataifa mawili ambapo Israel itaweza kuishi kwa usalama vilevile Wapalestina waweze kuwa na matumaini ya kupata maendeleo ya amani na kiuchumi. Hadi kulifikia lengo hilo, kuna mengi ya kufanya.´

Rais Abbas alikuwa mjini Berlin kupata uungwaji mkono kwa makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa taifa yaliyofikiwa baina ya chama cha Hamas na Fatah.

Baada ya kukutana hapo awali na waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, rais Abbas ametoa mwito mgomo dhidi ya serikali ya Palestina kufuatia ushindi wa kundi la Hamas kwenye uchaguzi wa bunge, umalizike.

Waziri Steinmeier alisisitiza sharti la pande nne zinazoudhamini mpango wa amani ya Mashariki ya Kati kwamba serikali mpya ya Palestina itatakikwa ilaani machafuko na iitambue haki ya kuwepo kwa taifa la Israel.

Rais Mahmoud Abbas ataendelea na safari yake ya kidiplomasia mjini Paris, Ufaransa.