BERLIN: Marufuku kuvuta kwenye vyombo vya usafiri wa umma | Habari za Ulimwengu | DW | 01.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Marufuku kuvuta kwenye vyombo vya usafiri wa umma

Kuanzia hii leo nchini Ujerumani ni marufuku kuvuta sigara katika vyombo vya usafiri vya umma na majengo ya serikali kuu.Wasiofuata sheria,watakabiliwa na faini ya hadi Euro 1,000.Vile vile umri wa kuweza kuvuta hadharani na kununua sigara umeongezwa kuwa miaka 18 badala ya 16.

Hata hivyo,sheria ya Ujerumani inawaruhusu wavutaji katika stesheni kubwa,kutumia sehemu au vyumba maalum vilivyowekwa kwa ajili yao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com