1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Madereva wa treni wagoma

8 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C791

Ulimwengu wa viwanda nchini Ujerumani unadaa mipango ya dharura kukabiliana na mgomo wa madereva wa treni nchini.

Maafisa wa bandari mjini Hamburg wameunda timu ya kukabiliana na hali ya dharura itakayotokana na hali hiyo. Kampuni ya meli ya Hapag-Lloyd imetangaza yumkini ikazipangia njia mpya meli zake au ikazitaka zisubiri baharini.Mgomo huo ambao umekusudia kulenga usafiri wa treni za mizigo unatazamiwa kuanza leo mchana na kudumu kwa masaa 42.

Chama cha wafanyakazi madereva wa treni GDL kimekataa pendekezo jipya la kuanza mazungumzo kutoka kwa shirika la reli la taifa Deutsche Bahn.Mgomo wa leo hii unatarajiwa kugharimu Deutsche Bahn hadi euro milioni 50 ikiwa ni hasara ya mapato kwa siku na unaweza kutibuwa uzalishaji kwenye viwanda vingi.

Chama cha wafanyakazi madereva wa treni kinadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 30.