BERLIN : Madereva wa treni kugoma leo hii | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Madereva wa treni kugoma leo hii

Chama kikuu cha wafanyakazi madereva wa treni nchini Ujerumani kimesema wanachama wake watagomea kazi kwa masaa matatu leo asubuhi.

Chama hicho cha wafanyakazi cha UDL kimeitisha mgomo huo kuunga mkono madai yao ya ongezekeo la asilimia 30 ya mshahara na mkataba tafauti wa ajira kutoka kwa wafanyakazi wengine wa reli.Vyama vyengine viwili vya wafanyakazi vilikubali ongezeko la mshahara la asilimia 4.5 kwa wafanyakazi wao miezi mitatu iliopita.

Shirika la reli la Ujerumani Deutsche Bahn limeahidi kuendelea kutowa huduma za usafiri wa masafa marefu kukabiliana na mgomo huo.

Wito wa mgomo huo unakuja masaa machache kabla ya mahkama ya kazi katika mji wa mashariki wa Chemnitz kutowa hukumu kwa ombi la Deutsche Bahn kuutangaza mgomo huo kuwa sio halali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com