1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Kansela Merkel asema Ulaya iko njia panda

2 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNK

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameonya kwamba Umoja wa Ulaya bado ungali unasua sua katika masuala muhimu ya dunia kama vile ukuaji wa uchumi na mabadiliko ya hali ya hewa.

Katika hotuba kwenye bunge mjini Berlin iliolenga juu ya sera ya serikali yake kwa Umoja wa Ulaya amesema Umoja wa Ulaya unawajibika kuonyesha kwamba ukuaji wa uchumi na mabadililiko ya hali ya hewa ni masuala yanayoweza kwenda sambamba. Hotuba yake hiyo inakuja kabla ya mkutano wa wiki ijayo wa viongozi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels ambapo Ujerumani ikiwa ni rais wa Umoja wa Ulaya inakusudia kupendekeza mabadiliko ya sera juu ya masuala ya hali ya hewa na pia kutowa wito wa kupunguzwa kwa urasimu.

Katika suala la biashara Merkel amesema Ujerumani itazidisha jitihada zake za kukamilishwa kwa mazungumzo ya biashara duniani ya duru ya Doha kutakakopelekea kufikiwa kwa makubaliano ya kuregeza masharti ya biashara duniani.