BERLIN: Kansela Angela Merkel ataendelea na sera za mabadiliko Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Kansela Angela Merkel ataendelea na sera za mabadiliko Ujerumani

Katika maadhimisho ya mwaka moja madarakani, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema mbele ya bunge kwamba serikali yake ya muungano itaendelea na mpango wa mabadiliko katika sera zake. Katika hotuba yake mbele ya bunge la Ujerumani, Bundestag, Merkel amesema ukuaji uchumi, kuongeza kodi ya mapato na kupunguza idadi ya wasiokuwa na kazi, vimeonyesha kuwa serikali anayoiongoza iko katika njia nzuri.

Kuhusu sera za maswala ya nchi za nje, Merkel amelaani mauaji ya waziri wa viwanda wa Lebanon, Pierre Gemayel na kwamba Ujerumani inaunga mkono uhuru wa Lebanon. Amezungumzia pia jukumu la wanajeshi wa Ujerumani walioko nchini Lebanon katika kikosi cha Umoja wa mataifa cha kulinda amani na vile vile nchini Afghanistan. Lakini Merkel, ametupilia mbali wito uliotolewa na Marekani na jumuiya ya NATO kwamba wanajeshi wa Ujerumani wangetawanywa pia katika eneo lenye machafuko la kusini mwa Afghanistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com