BERLIN : Kambi ya Marekani yatishiwa kushambuliwa | Habari za Ulimwengu | DW | 11.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Kambi ya Marekani yatishiwa kushambuliwa

Polisi ya Ujerumani imeanzisha operesheni kubwa katika kambi ya kijeshi ya Marekani huko Spangdahlem magharibi ya Ujerumani baada ya wanajeshi wa Marekani kupokea vitisho kwa njia ya simu.

Hapo jana jioni mtu asiejulikana aliwapigia simu na kusema kwamba yeye na wenzake wanne wataishambulia kambi hiyo kwa mabomu.Polisi inasema alikuwa akizungumza lugha ya Kijerumani yenye lahaja ya kigeni yumkini akiwa ni Mrusi au Mturuki.

Operesheni hiyo inakuja katika kipindi kisichozidi wiki moja kufuatia kukamatwa kwa watuhumiwa watatu kwa tuhuma za kupanga mashambulizi kwa viwanja vya ndege na sehemu nyengine zinazotembelewa sana na Wamarekani hapa nchini Ujerumani lakini polisi hawakuweza kuthibitisha iwapo matukio haya yana uhusiano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com