1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Hakuna maafikiano kuhusu tarehe mpya

17 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaA

Mpatanishi mkuu wa Marekani,Christopher Hill alikuwa na mazungumzo yasio rasmi pamoja na naibu waziri wa kigeni wa Korea ya Kaskazini,Kim Kye Gwan katika mji mkuu wa Ujerumani,Berlin kuhusika na mradi wa nuklia wa Korea ya Kaskazini.Lakini hakuna maafikiano yaliopatikana juu ya tarehe mpya ya kuendelea na majadiliano ya pande sita kuhusu mradi wa nuklia wa Korea ya Kaskazini uliozusha mabishano.Duru ya mwisho ya majadiliano kuhusu mradi wa nuklia wa Pyongyang ilikuwa mwezi wa Desemba.Majadiliano hayo yalimalizika bila ya kupatikana maendeleo yo yote.