BERLIN: Bunge la Ujerumani laidhinisha ndege zipelekwe Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 09.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Bunge la Ujerumani laidhinisha ndege zipelekwe Afghanistan

Bunge la Ujerumani, Bundestag, limeidhinisha uamuzi wa serikali wa kutuma ndege sita aina ya tornado kwenda nchini Afghanistan na kuongeza wanajeshi 500 zaidi nchini humo.

Mpango huo ulikosolewa vikali na wanasiasa wa upinzani.

Ndege za tornado zitatumiwa kupigia picha maeneo wanakojifidha waasi wa Taliban na kuliwezesha jeshi la ISAF linaloongozwa na shirika la kujihami la kambi ya magharibi NATO kupanga operesheni zake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com