BERLIN: Bundestag yaidhinisha mswada kupunguza kodi ya pato | Habari za Ulimwengu | DW | 25.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Bundestag yaidhinisha mswada kupunguza kodi ya pato

Bunge la Ujerumani(Bundestag)limepitisha mswada unaopendekeza kupunguza kodi ya pato ya makampuni kutoka asilimia 39 hadi asilimia 30.Jamii ya wafanyabiashara ina matumaini kuwa hatua hiyo itavutia Ujerumani uwekezaji zaidi wa kigeni. Ujerumani ni nchi inayotoza kodi kubwa kabisa barani Ulaya.Mswada huo ukipitishwa na baraza la mabunge ya mikoa(Bundesrat),basi sheria itaanza kutumika mapema mwakani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com