1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Beck apinga awamu ya pili katika serikali ya mseto

29 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBe1

Kiongozi wa chama cha SPD nchini Ujerumani amesema,atapinga chama chake kushiriki katika serikali ya mseto pamoja na chama cha CDU cha Kansela Angela Merkel kwa awamu ya pili.

Kurt Beck ameliambia gazeti la “Bild am Sonntag“ kuwa hiyo haitokuwa busara kwa demokrasia,nchini Ujerumani.Akasema,vyama vikuu viwili,baada ya kupatikana matokeo ya uchaguzi mkuu katika mwaka 2005,havijakuwa na chaguo jingine isipokuwa kufanya kazi pamoja.Akaongezea kuwa vyama hivyo viwili hata hivyo,huweza kuafikiana katika masuala machache.