1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bemba akamatwa.

Mtullya, Abdu Said25 Mei 2008

Aliekuwa makamu wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Jean-Pierre Bemba amekamatwa mjini Brussels.

https://p.dw.com/p/E5ZT
Aliekuwa makamu wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya KongoPicha: AP

Aliekuwa makamu wa  rais nchini Jamhuri ya  Kidemokrasi ya Kongo Jean -Pierre Bemba   amekamatwa

Bemba  ambae pia alikuwa  kiongozi wa waasi  alikamatwa karibu na mji mkuu wa  Ubelgiji Brussels   jana  kutokana kufuatia  ombi  la mahakama ya kimataifa inayopambana  na uhalifu ICC ya mjini  the  Hague.

Mwendesha mashataka  wa mahakama hiyo  ameliambia shirika la habari  la AFP, kuwa mahakama  ya ICC sasa inaisubiri serikali  ya  Ubelgiji itoe amri  ili mwanasiasa  huyo  apelekwe mjini  The Hague kujibu  mashtaka manne juu ya uhalifu wa  kivita  na mawili ya uhalifu dhidi ya  ubinadamu.

Mnamo  miezi  ya hivi karibuni Bemba alikuwa anaishi   katika  hifadhi  ya kisiasa nchini Ureno  baada  ya kushindwa katika  uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya  Kidemokrasi ya Kongo  miaka  miwili  ilyopita.

Bemba pia anakabiliwa na shtaka la uhaini nchini  mwake.