1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BELGRADE:Mahafidhina washinda uchaguzi mkuu Serbia

Chama cha chenye msimamo mkali huko Serbia, kimejitangaza kushinda katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Chama hicho kimesema kuwa matokeo ya uchaguzi huo uliyofanyika jana yanaonesha kukataa kwa wananchi kuwa na uhusiano na watuhumiwa wa mauaji ya Kosovo.

Hata hivyo kimekiri kuwa hakitakuwa na uwezo wa kuunda serikali kutokana na idadi ya viti bungeni.

Matokeo yanaonesha kuwa chama hicho cha upinzani chenye msimamo mkali, kinaongoza kwa asilimia 28, huku chama chenye kuegemea Ulaya cha Democratic kikikamata nafasi ya pili kwa kuwa na asilimia 23.

Wakati huo huo matokeo ya uchaguzi huo yaligubika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa umoja wa Ulaya unaoendelea hivi sasa mjini Brussels Ubelgiji.

Waziri wa mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeir anaongoza mkutano kwa mara ya kwanza toka Ujerumani ilipochukua kiti cha urais wa umoja huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com