1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Belgrade. Waserbia kuidhinisha katiba mpya.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCy8

Upigaji kura umeanza nchini Serbia kwa siku ya pili na ya mwisho katika kura ya maoni juu ya katiba mpya.

Idadi ya watu waliojitokeza jana Jumamosi inasemekana kuwa ndogo ikiwa ni chini ya asilimia 18.

Kiasi cha zaidi ya watu milioni 6 wana haki ya kupiga kura na zaidi ya nusu ya idadi hiyo walitakiwa kupiga kura ya ndio ili katiba hiyo iweze kuidhinishwa.

Muswada huo mpya wa katiba unatamka kuwa jimbo la Kosovo ni sehemu ya Serbia, licha ya madai ya jimbo hilo linalotaka kujitenga kutaka kujitangazia uhuru.

Uchaguzi mpya utafuatia nchini Serbia , iwapo katiba hiyo itaidhinishwa.