1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Belfast:Uchaguzi katika jimbo la Ireland kaskazini

7 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLY

Wakaazi wa jamii mbili za Ireland kaskazini-wakatoliki na waprotestanti- wanapiga kura leo, katika uchaguzi unaotarajiwa kufungua njia ya kugawana madaraka kati ya jamii hizo mbili. Uchaguzi wa bunge la Ireland kaskazini unaangaliwa kama ni hatua moja mbele katika kurejesha tena utawala katika mkoa huo wa Uingereza wenye mnatatizo, ikiwa ni miaka mine baada ya kusimamishwa na mamlaka kurudishwa kwa serikali mjini London, baada ya kuzuka hali ya kutoaminiana kati ya jamii hizo mbili.

Ni mara ya 10 ambapo wapiga kura milioni moja na laki moja wa Ireland kaskazini wanapiga kura, tangu mkataba wa amani wa Aprili 1998, ambao kwa sehemu kubwa umemaliza miaka 30 ya umwagaji damu. Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair anatazamiwa kukutana na mwenzake wa Jamhuri ya Ireland Berti Ahern mnamo siku ya Ijumaa kuzungumzia matokeo ya kwanza ya uchaguzi huo. Uingereza na jamhuri ya Ireland zinashirikiana katika kusaka ufumbuzi wa kudumu wa mzozo wa Ireland kaskazini.