1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Lebanon yawataka wapiganaji wa kiislam wajisalimishe

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByx

Waziri wa ulinzi wa Lebanon Elias Murr, amesema kuwa wapiganaji wa kundi la Fatah al Islam waliyochimbia katika kambi ya wapalestina, ni lazima wajisalimishe vinginevyo watakabiliana na mashambulizi mengine zaidi ya kijeshi.

Amesema kuwa jeshi la Lebanon kamwe halitakuwa na majadiliano na magaidi na wahalifu.

Mapema maelfu ya wakimbizi walitumia mwanya wa kusitishwa kwa mapigano kukimbia.

Zaidi ya watu 80 wameuawa toka kuzuka kwa mapigano hayo siku ya jumapili.

Katika mji wa milimani wa Druze uliyoko mashariki mwa Beirut, watu watano wamejeruhiwa kutokana na mlipuko wa bomu.