BEIRUT: Wanamgambo washambuliwa kambi ya Nahr al-Bared
9 Juni 2007Matangazo
Nchini Lebanon,vikosi vya serikali vimeshambulia tena vituo vya wanamgambo wa Fatah al-Islam waliojificha katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nahr-al-Bared.Wanamgambo hao,tangu majuma kadhaa sasa,wanajificha katika kambi hiyo,kaskazini mwa Lebanon.Mashahidi wamesema, kambi hiyo imeshambuliwa na kama maguruneti 20 yaliosababisha moto.