BEIRUT: Wahezbollah wataka kubadilishana wafungwa
29 Julai 2007Matangazo
Nchini Lebanon,kiongozi wa chama cha Hezbollah chenye sera kali amesema wanajeshi 2 wa Kiisraeli waliotekwa nyara mwaka mmoja uliopita wataachiliwa huru kwa kubadilishana wafungwa tu. Sheikh Hassan Nasrallah,alitamka hayo katika hotuba yake kwenye televisheni.Chama cha Hezbollah kiliwateka nyara wanajeshi hao wawili Julai mwaka jana,hatua iliyoifanya Israel kuanzisha vita vya mwezi mmoja dhidi ya Hezbollah.