BEIRUT : Waendelea kushinkiza kun’gatuka kwa serikali | Habari za Ulimwengu | DW | 02.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT : Waendelea kushinkiza kun’gatuka kwa serikali

Maelfu ya wafuasi wa Hezbollah leo hii wameendelea kupiga kambi katikati ya jiji la Beirut wakati kundi hilo la wapiganaji wa Kiislam la Washia na washiria wake wakiendelea kushinikiza kujiuzulu kwa serikali ya Fouad Siniora inayoungwa mkono na Marekani.

Maafisa wa Hezbollah wanasema kampeni yao hiyo ambayo imetibuwa maisha kwenye eneo hilo la kibiashara mjini Beirut haitosita hadi hapo yatakapotimizwa madai yao ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.Serikali haikuonyesha ishara ya kusalimu amri katika malumbano ambayo yanaweza kuripuka kuwa umwagaji damu na kuivuruga nchi hiyo.

Inakadiriwa kwamba watu waliojitokeza kwenye maandamano hayo hapo jana wanafikia 800,000 ambayo ni sawa na theluthi moja ya idadi ya watu nchini Lebanon.

Maandamano hayo hadi sasa yamekuwa yakifanyika kwa amani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com