1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Umwagaji damu waendelea Ukanda wa Gaza

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsT

Wafanyakazi 2 wa tawi la Shirika la Mslaba Mwekundu nchini Lebanon,wameuawa katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Nahr al-Bared kaskazini mwa nchi.Kwa mujibu wa msemaji wa tawi hilo,Georges Kettane,wafanya kazi hao wawili walipigwa na risasi walipokuwa wakimshindikiza msomi wa Kiislamu kwenye kambi hiyo ya wakimbizi, kujaribu kupata maafikiano ya kukomesha mapigano. Wanajeshi 3 pia waliuawa,katika ufyatuaji wa risasi.Hapo awali,sehemu za kaskazini na mashariki za Nahr al-Bared zilishambuliwa na vikosi vya Lebanon.Wanamgambo wa kundi la Fatah al-Islam wanajificha katika kambi hiyo tangu tarehe 20 mwezi Mei.