BEIRUT: Majadiliano ya kuunda serikali ya umoja yavunjika
12 Novemba 2006Matangazo
Mgogoro wa kisiasa nchini Lebanon umezidi kuwa mkali.Waziri mkuu Fuad Siniora amekataa kukubali kujiuzulu kwa mawaziri watano wa Kishia. Inasemekana kwamba madai ya mawaziri hao kutaka makundi ya Hezbollah na Amal,yanayoiunga mkono Syria kuwa na usemi zaidi bungeni, hayakutimizwa.Stesheni ya televisheni ya Washia- Al Manar-imeripoti kuwa majadiliano yalioitishwa na Hezbollah,kuunda serikali ya umoja wa taifa yamevunjika.