BEIRUT : Maelfu wahudhuria mazishi ya mbunge alieuwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT : Maelfu wahudhuria mazishi ya mbunge alieuwawa

Maelfu ya wananchi wa Lebanon leo wamehudhuria mazishi ya mbunge aliekuwa akiipinga Syria Antonio Ghanem mjini Beirut.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mauaji ya Ghanem katika mripuko wa gari hapo Jumaatano na limedai kukomeshwa mara moja kwa mauaji yanayowalenga wanasiasa wa Lebanon.Watu wengine sita waliuwawa kwenye mripuko huo wa bomu uliotokea kwenye kitongoji cha Beirut.Mripuko huo umetokea siku chache tu kabla ya bunge kumchaguwa mtu wa kuchukuwa nafasi ya Rais Emile Lahoud.

Spika wa bunge Nabih Berri amesema uchaguzi huo utafanyika kama ilivyopangwa hapo Jumanne.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com