1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Olmert kuzuru China

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcO

Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert anatarajiwa kuwasili kesho mjini Beijing China katika awamu yake ya mwisho ya ziara yake ya mataifa matano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Waziri Olmert anazuru China huku juhudi za kuumaliza mzozo wa nyuklia wa Iran zikiendelea. Olmert anatarajiwa pia kutafuta njia za kuboresha ushrikiano wa kiuchumi na China.

Maofisa hawatarajii pendekezo la Olmert kuiwekea vikwazo vikali Iran kuunguwa mkono nchini China kama ilivyokuwa nchini Uingereza, Ufaransa, Urusi na Marekani.