BEIJING: Majadiliano kuhusu mradi wa nyuklia wa Korea Kaskazini | Habari za Ulimwengu | DW | 08.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING: Majadiliano kuhusu mradi wa nyuklia wa Korea Kaskazini

Duru mpya ya mazungumzo ya kundi la pande sita yameanza mjini Beijing.Lengo la majadiliano hayo yanayohudhuriwa na China,Japan,Urussi,Marekani, Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini ni kuishawishi Korea ya Kaskazini kuachilia mbali mradi wake wa nyuklia.Oktoba mwaka jana,hali ya wasi wasi iliongezeka baada ya serikali ya Pyongyang kufanya jeribio lake la kwanza la nyuklia.Siku chache baadae,Umoja wa Mataifa ukachukua hatua ya kuiwekea vikwazo Korea ya Kaskazini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com