1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING: Majadiliano kuhusu Korea ya Kaskazini yataendelea juma lijalo

11 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCT7

Duru mpya ya majadiliano ya kundi la pande sita mjini Beijing,kuhusu mradi wa kinyuklia wa Korea ya Kaskazini imemalizika bila ya kupata makubaliano.Baada ya mazungumzo ya siku nne, mpatanishi wa Japan Kenichiro Sasae amesema, majadiliano hayo yataendelea wiki ijayo.Akaongezea kuwa madai makuu ya Korea ya Kaskazini yanachelewesha kufikia maafikiano. Kwa mujibu wa vyombo vya habari,Korea ya Kaskazini itasitisha mpango wake wa kinyuklia ikiwa tu kila mwaka itapatiwa tani milioni 2 za mafuta na vile vile kilowati milioni 2 za umeme. Mbali na Korea ya Kaskazini,Japan na China, majadiliano hayo mjini Beijing yanahudhuriwa pia na Urussi,Marekani na Korea ya Kusini.