BEIJING: Korea ya Kaskazini imeashiria itayari kufunga mitambo yote | Habari za Ulimwengu | DW | 19.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIJING: Korea ya Kaskazini imeashiria itayari kufunga mitambo yote

Maafisa kutoka China,Urusi,Japan,Marekani na Korea zote mbili wamerefusha majadiliano yao mjini Beijing hadi siku ya Ijumaa.Lengo ni kuipangia Korea ya Kaskazini ratiba ya kufunga mitambo yake yote ya nyuklia.Wajumbe hao wa kimataifa wanasema,Korea ya Kaskazini imeashiria kuwa ipo tayari kuifunga mitambo yake yote ya nyuklia mwaka huu.Siku ya Jumatano,mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomu la Umoja wa Mataifa,bwana Mohammed ElBaradei alithibitisha kuwa mitambo mitano mikuu ya nyuklia ya Korea ya Kaskazini imeshafungwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com