Bayern, Chelsea na kibarua cha barani Ulaya
9 Machi 2015Matangazo
Chelsea, iliyoshinda Kombe la 2012, ilipata goli la ugenini katika sare ya 1-1 na Paris St Germain wakati mabinhwa wa 2013 Bayern Munich wakitoka sare ya bila na Shakhtar Donetsk mjini Lviv.
Kesho Jumanne, Porto itakutana na Basel baada ya sare ya 1-1 nchini Uswisi wakati Real Madrid wakitaraji kuwa faida yao ya mabao mawili kwa sifuri itatosha kuwapa tikiti ya robo fainali nyumbani kwa Schalke.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP/reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman