1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BASTI ABDULLAH, Pakistan:Abdul Rashid Ghazi azikwa

12 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjT

Takriban watu alfu 2 wanahudhuria mazishi ya kiongozi wa kidini aliye na msimamo mkali wa Taliban Abdul Rashid Ghazi aliyeuawa wakati msikiti mwekundu uliposhambuliwa na jeshi la Pakistan.

Kakake ,Abdul Aziz ambaye ni kiongozi wa Lal Masjid aliyekamatwa wiki jana pamoja na jamaa zake waliruhusiwa kuhudhuria shughuli hiyo.

Polisi wanashika doria katika eneo hilo ili kudhibiti usalama ili kuzuia ulipizaji kisasi kutoka kwa wafuasi wa msikiti huo.

Rais Pervez Musharraf anatarajiwa kuhutubia taifa hii leo kueleza umuhimu wa hatua iliyochukuliwa ya kuvamia Msikiti wa Lal na madrassa ya watoto wa kike iliyokuwa karibu vilevile kupambana na ugaidi.

''

Tuliposhambulia msikiti na kuudhibiti sasa wanatoroka katika vikundi vidogo kuelekea maeneo ya milimani.Kwahiyo tumevunjilia mbali mizizi yote ya kundi hilo.''

Wakati huohuo naibu kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda Ayman al Zawahri anatoa wito kwa waislamu nchini humo kuendelea na Jihad ili kupinga serikali.

Msikiti huo ulitekwa baada ya ghasia kuzuka mwanzoni mwa mwezi huu kati ya polisi na wanafunzi wa msikiti huo walio na msimamo mkali.