1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BASRA: majeshi ya Uingereza yawakoa mahabusu katika hatari ya kuawa

Majeshi ya Uingereza huko Iraq yamevamia makao makuu ya polisi katika mji wa kusini mwa Iraq, Basra baada ya kuwepo taarifa kuwa maafisa wa kituo hicho walikuwa mbioni kuwaua mahabusu 178.

Msemaji wa jeshi hilo la Uingereza huko Iraq, Meja Charlie Burbridge amesema kuwa kikosi maalum cha polisi cha kupambana na uhalifu kinatavunjwa.Kikosi hicho yaarifiwa kuwa ndicho kilichokuwa kifanye mauaji hayo.

Msemaji huyo amesema kuwa , majeshi ya Uingereza yakishirikiana na yale ya Iraq, yalifanikiwa kuwaachia wafungwa 76, kutoka katika kituo hicho cha polisi cha Jamatiya huko Basra.

Vyombo vya habari vimeharifu kuwa, kulikuwa na uharibifu wa nyumba na magari jirani na kituo hicho wakati wa uokoaji huo.

Huko Ramadi mshambuliaji wa kujitoa mhanga amejilipua katika kituo cha polisi na kuua askari polisi watatu na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Polisi wanasema mtu huyo aliingia katika mlango kwenye kituo cha polisi kilichoko kwenye chuo kikuu cha mji huo wa Ramadi na kujilipua

Wakati huo huo majeshi ya Marekani nchini Iraq yanawashikilia raia wanne wa Iran ambao walikuwa mjini Baghdad kwa mwaliko war ais Jalal Talabani wa Iraq.

Watu hao wanne ambao ni pamoja na mamafisa wa ngazi za juu wa Iran wanatuhumiwa na Marekani kuwa walikuwa nchini Iraq kutekeleza mipango ya mashambulizi.

Hata hivyo kwa mujibu wa mshauri wa habari war ais Jalal,Hiwa Osman, rais huyo wa Iraq amechukizwa na kitendo hicho cha majeshi ya marekani.

Amesema kuwa watu hao walialikwa ikiwa ni katika mikakati ya makubaliano kati ya Iran na Iraq katika kuimarisha hali ya uslama nchini Iraq ambayo ni mbaya sana.

Majeshi ya Marekani yaliwakamata watu hao wanne wakiwemo maafisa wawili wa kibalozi wa Iran na baadae kuwaachia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com