Basra, Iraq. Uingereza kuongeza msaada wake Iraq. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Basra, Iraq. Uingereza kuongeza msaada wake Iraq.

Uingereza imesema kuwa inampango wa kuongeza msaada kwa Iraq kwa kiasi cha Euro milioni 150 katika muda wa miaka mitatu ijayo.

Waziri wa fedha wa Uingereza Gordon Brown ametoa taarifa hiyo wakati wa ziara yake kusini mwa Iraq katika mji wa Basra.

Baada ya kwenda nchini humo akitokea Kuwait, Brown alikutana na kundi dogo la wanajeshi katika kituo cha kijeshi cha Uingereza katika mji huo.

Uingereza ina kiasi cha wanajeshi 7,000 kusini mwa Iraq.

Brown anaonekana kuwa katika nafasi ya mbele kuweza kuchukua wadhifa alionao waziri mkuu wa sasa Tony Blair, ambaye anatarajiwa kung’atuka madarakani mwezi May mwakani.

Ziara yake inakuja siku moja baada ya Tony Blair kutumia neno , maafa , kuelezea hali nchini Iraq kufuatia uvamizi ulioongozwa na majeshi ya Marekani.

Blair ambaye ametoa maelezo hayo katika mahojiano na shirika la utangazaji la Al-Jazeera, ameongeza kuwa Uingereza haiwezi kujiondoa kutoka katika nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com